WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumatano, Agosti 16, 2017)
kuelekea nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la
kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Akiwa nchini Cuba Waziri Mkuu anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Cuba kwa lengo la kukuza ushirikiano katika sekta za afya, elimu utalii na Kilimo.
Aidha, nchi ya Cuba ni mojawapo ya nchi zenye ushirikano wa muda mrefu na Tanzania Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Felex
Jackson katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Dar es salaam leo
August,16/2017 akiwa anaelekea Nchini Cuba Kwa ziara ya kikazi.Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 16, 2017.
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 16, 2017.
Comments
Post a Comment