
Mawe yakiwa yamepangwa barabarani wakati polisi wakiimarisha usalama.
Watu
wawili wameuawa wakati wa vurugu akikabiliana na maofisa wa polisi
katika ngome ya upinzani ya Mathare, Mji Mkuu wa Nairobi nchini Kenya.

Risasi zikilindima.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa walisikia milindimo ya
risasi zikifyatuliwa wakati wa makabiliano hayo ambayo yalisababisha
vifo hivyo.

Polisi wakituliza ghasia.
Afisa
Habari wa Shirika la Habari la Uransa, Agence France-Presse (AFP),
limeeleza kuwa, waliouawa walikuwa miongoni mwa kundi la waandamanaji
katika eneo hilo ambao walikuwa wakipambana na kikosi maalum cha kuzuia
ghasia hizo.

Hali ilivyokuwa.
”Tumeambiwa kwamba wengi wao walikuwa wezi ambao walitumia fursa hiyo na hawakuweza hata kuwaheshimu polisi”, alisema ofisa huyo.

Askari wakituliza ghasia.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa uchaguzi huo umefanyiwa udanganyifu ili kumpokonya ushindi.
Mataili yakichomwa barabarani.
Comments
Post a Comment