UCHAGUZI KENYA: ODINGA, KENYATTA WAPIGA KURA


Kenyatta akipiga kura
LEO ni siku ya uchaguzi nchini Kenya na Wakenya wengi wamejitokeza kupiga kura. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa 11:00 asubuhi. Mpaka sasa, wagombea wanaochuana vikali, Odinga na Kenyatta, wamepiga kura katika maeneo tofauti.
Odinga akipiga kura.
Rais Uhuru Kenyatta amepiga kura kwenye shule ya msingi ya Mutomo na amesikika akiwaomba Wakenya wote wafanye uchaguzi huo kwa amani.
Kenyatta akipiga kura.
Upande mwingine, Odinga amepiga kura katika shule ya Kibra, Nairobi. Ikumbukwe kuwa Odinga anagombea kwa mara ya nne sasa.
Habari zaidi kinachoendelea katia uchaguzi huo zitaendelea kukufikia hapahapa.


Comments