Katibu wa Chama Cha Mpira Wilaya ya
Bukombe Bw. Bosco Mwidadi akizungumza na wachezaji wa Timu ya Young Boys kutoka Kata Bulangwa na Silamila Fc inayowakilisha Kata ya Butinzya katika viwanja vya Shule ya Sekondari Butinzya katika mchezo wa fainali ya ngazi ya Tarafa ya Ushirombo kwenye michuano ya Ligi ya Doto Cup 2017
Timu ya Young Boys Fc iliyopo Kata ya Bulangwa kwa pamoja wakimsikiliza kocha wao wakati akitoa mbinu za kupata ushindi kabla ya mchezo kuanza.
Timu ya Silamila Fc inayowakilisha Kata ya Butinzya wakiwa katika picha ya pamoja kabla mchezo kuanza.
Timu ya Young Boys Fc iliyopo Kata ya Bulangwa kwa pamoja wakimsikiliza kocha wao wakati akitoa mbinu za kupata ushindi kabla ya mchezo kuanza.
Timu ya Silamila Fc inayowakilisha Kata ya Butinzya wakiwa katika picha ya pamoja kabla mchezo kuanza.
Kama kawaida yetu mashabiki.
Timu
ya Young Boys Fc iliyopo Kata ya Bulangwa Wilayani Bukombe Mkoani
Geita jana imejinyakulia ushindi baada
ya kuichapa gori 2-0 Timu ya Silamila Fc inayowakilisha Kata ya Butinzya katika
hatua ya fainali ngazi ya Tarafa katika
ligi ya Doto Cup 2017 iliyohitimishwa hapo jana katika uwanja wa Shule
ya Sekondari Butinzya.
Mechi hiyo iliyohudhuliwa na mamia ya
mashabiki katika uwanja wa Shule ya Sekondari Butinzya ,Timu ya Young
Boys ilichapa gori la kwanza Timu ya Silamila Fc dakika ya 52 kupitia kwa kiungo mshambuliaji Gasper Joseph
na gori la pili kupitia kwa Omary Shavi dakika ya 69.
Hadi dakika tisini ya mchezo huo Timu ya Silamila fc haikupata hata gori
la kufutia chozi.
Katibu wa Chama Cha Mpira Wilaya ya
Bukombe Bw. Bosco Mwidadi amezipongeza timu zote zilizojitokeza kushiliki ligi
hiyo iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la
Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko na kutoa rai kwa mashabiki na wadau wote wa
mpira wazidi kujitokeza viwanjani kwani vipaji vya vijana wa Bukombe vinazidi
kudhihirika viwanjani.
Comments
Post a Comment