
Rais Museveni akikagua nyaraka zake za Ubatizoa.
Kwa
muda mrefu sana kumekuwa na mijadala hasa katika mitandao ya kijamii
nchini Uganda kuhusu umri halisi wa Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta
Museveni.
Kwa
mara kadhaa serikali ya Uganda imekuwa ikinukuliwa ikisema kwamba Rais
Museveni alizaliwa mwaka 1944, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka
jana vyama vya upinzani vilikuwa vikimkosoa Rais Museveni kwamba
anadanganya kwa kusema ana miaka 71. Vyama hivyo vilidaiwa kuwa alikuwa
na zaidi ya umri wa miaka 75 na asingeweza kugombea tena.

…Akiwa na mkewe na viongozi wa kanisa.
Lakini
mjadala mpya umeibuka ambapo Ikulu ya Uganda imechapisha nyaraka kwenye
ukurasa wake wa Facebook zinazoonyesha kwamba nyaraka za ubatizo wa
Rais zimeandikwa tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni 3 Agosti 1947 na
hivyo sasa ana miaka 70.
Kwa
minajili hiyo, Rais Museveni atakuwa na umri wa maika 74 wakati Uganda
itakapofanya uchaguzi mwingine mwaka 2021 na hivyo ataweza kugombea tena
katika awamu ya sita.

Nyaraka zake za Ubatizo zilizotolewa na Ikulu ya Uganda.
Museveni
alibadilisha katiba ya Uganda mwaka 2006 ili kuweza kugombea awamu ya
tatu. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini humo, Rais amewahi
kusema kwamba hafahamu tarehe yake ya kuzaliwa.
“Wazazi
wangu hawakwenda shule na hivyo hawakujua tarehe,” alinukuliwa Rais
Museveni mwaka 1997 alipokuwa akitoa taarifa zake katika mahojiano
maalum.

Nyaraka zake za Ubatizo zilizotolewa na Ikulu ya Uganda.
Mkanganyiko
huu umekuja ikiwa ni takribani wiki moja tangu Rais Museveni aliposema
kuwa katika kipindi cha miaka 31 alichokuwa madarakani hajawahi kuugua.
“Umewahi
kusikia Museveni ameumwa na miguu yake kuning’inizwa hospitalini kwa
miaka 31 iliyopita? Hii ni kwa sababu nafuata hatua za msingi za afya
ambazo zimenisaidia kuepukana na magonjwa. Magonjwa haya yanaweza
kuzuilika,” alisema Museveni akitamba kwamba afya yake ni imara.
Comments
Post a Comment