
Mtoto wa
miezi sita aliyejeruhiwa na maafisa wa polisi baada ya kutangazwa kwa
matekeo ya uchaguzi yaliozua utata nchini Kenya amefariki, kulingana na
familia yake.Samantha
Pendo alikuwa katika hali mahututi tangu siku ya Ijumaa baada ya kupata
majeraha ya kichwa wakati polisi walipovamia nyumba yao katika mtaa wa
mabanda magharibi mwa mji wa Kisumu
Babake
Joseph Abanja , aliambia gazeti la Daily Nation: Nataka haki kwa
mwanangu.hakuwa akiandamana , babake hakuwa akiandamana pia.Mamake
hakuwa akiandamana na badala yake walimuua.
''Nilifanya nilivyoambiwa kwenda kupiga kura na kurudi nyumbani''.Walitufuata hapa na kutupiga''.
Takriuban
watu 24 waliuawa katika ghasia ambazo zilizuka baada ya uchaguzi wa
tarehe 8 mwezi Agosti kulingana na shirika moja la haki za
kibinaadamu''.
Kiongozi
wa upinzani Raila Odinga alisema kuwa uchaguzi huo ulifanyiwa
udanganyifu ili kumsaidia rais aliyepo madarakani Uhuru kenyatta
kushinda.
Hatahivyo wachunguzi wa kimataifa wanasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
Comments
Post a Comment