MHE. DOTO BITEKO AMALIZA CHANGAMOTO ZA SHIKALIBUGA-BUKOMBE

  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akikata utepe kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Shikalibuga- Businda.
  Wanakazi wa Shikalibuga wakiwa na  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa pamoja wakielekea eneo la Mkutano.
  Mtumishi wa Mungu akifungua Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa Maombi.
 
  Diwani wa Kata ya Ushirombo akizungumza na wakazi wa Shikalibuga kwenye Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.


  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Ushirombo Mhe. Lameck Warangi.

  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wakazi wa Shikalibuga na Viunga vyake.
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na wananchi waliyojitokea kuuliza maswali.

   Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akimwombea msamaha moja ya Mkazi wa Shikalibuga(mwenye shati ya mistari myekundu) baada ya Kutengwa kwa muda mrefu kwa kosa la utovu wa nidhamu kwa viongozi wa ngazi ya kijiji hicho.
  


Wakazi  wa Kijiji cha Shikalibuga kilichoko Kata ya Ushirombo Wilayani Bukombe  kwa ujumla bila kujali itikadi dini wala ukabila imetakiwa kuishi kwa amani na upendo mkubwa huku wakiheshimiana baina ya wakulima na wafugaji ili kuondoa migogoro yao na kujiletea maendeo kwa kutumia vizuri rasili mali zao.

Rai hiyo ilitolewa na  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko  wakati akizunguza na wakazi wa Shikalibiga na viunga vyake alipokwenda kwa ajili ya uzinduzi wa barabara ya Shikalibuga  – Businda yenye urefu wa kilimita nne kiwango cha moramu.
   
Pia alimshukuru Mkandarasi kwa kazi aliyoifanya na kumsihi  Diwani wa Kata hiyo Mhe. Lameck Warangi fuatilia kwa karibu ili kihakikisha mkandarasi huyo analiboresha barabara hilo kwa kulishindilia vizuri.

Kwa Upande wake  Diwani wa Kata ya Ushirombo Mhe. Lameck Warangi aliwasihi wananchi hao kuachana na siasa za Januari hadi Desemba na badala yake watumie mda wao vizuri na kufanya kazi kwa maendeleo yao sambamba na kuziunga mkono jitihada za Mbunge wao Mhe. Biteko na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ili kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.  



Comments