JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA KUCHUNGUZA CHANZO CHA VURUGU ZILIZOTOKEA MTAA WA MABATINI WILAYANI NYAMAGANA.
KWAMBA
TAREHE 08.08.2017 MAJIRA Y A SAA 22:00 USIKU KATIKA MTAA WA MABATINI
KATA YA MABATINI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA
T.394 DJW AINA YA TOYOTA HAICE AMBALO LINADAIWA LILIKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA AMINI SHABANI SIZYA MIAKA 28,
MNYAMWEZI, MKAZI WA MTAA WA MABATINI. INASEMEKANA KUWA DEREVA WA GARI
HILO WAKATI ALIPOKUWA MAHALI HAPO ALIGEUZA GARI LAKINI ENEO LILIKUWA
FINYU HIVYO ALIKWENDA KUGONGA NYUMBA (PUB) ILIYOKUWA PEMBENI MALI YA
BONIFACE NTOBI NA KUVUNJA UKUTA NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI NA VITU
VYENYE KIASI CHA THAMANI YA TSH 4,000,000/=.
INASEMEKANA
KUWA BAADA YA TUKIO HILO KUTOKEA WANANCHI WALITOA TAARIFA KITUO CHA
POLISI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA
KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA DEREVA WA GARI HILO,
LAKINI IKATOKEA KUTOELEWANA KATI YA ASKARI WENGINE WALIOFIKA ENEO HILO
NA MWENYE NYUMBA (PUB) PAMOJA NA WANANCHI NA KUPELEKEA KUZUKA KWA VURUGU
AMBAPO WANANCHI WALIANZA KUWARUSHIA ASKARI MAWE NDIPO ASKARI WALIFYATUA
RISASI KADHAA HEWANI HALI ILIYOPELEKEA HOFU KWA WANANCHI WA ENEO
HILO.
KATIKA
VURUGU HIZO MKE WA MWENYE NYUMBA (PUB) BI BETI ATANASI ALIJERUHIWA MGUU
WA KULIA JUU YA UNYAYO, LAKINI BADO HAIJATHIBITIKA KUWA JERAHA HILO NI
LA KITU GANI KWANI MAJERUHI ANAONGEA NA ANAWEZA KUTEMBEA YUPO HOSPITALI
YA RUFAA YA BUGANDO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HIVYO TUNASUBIRI
UCHUNGUZI WA KISAYANSI WA DAKTARI ILI KUWEZA KUTHIBITISHA JUU YA JERAHA
HILO.
AIDHA
KUFUATIA VURUGU ZILIZOTOKEA KATIKA ENEO HILO NA KUSABABISHA ASKARI
KUFYATUA RISASI. JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEANZA UCHUNGUZI WA
SUALA HILO ILI KUBAINI CHANZO HALISI CHA VURUGU HIZO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA
WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA KUTULIA WAKATI
JESHI LIKIENDELEA NA UCHUGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO. AIDHA PIA
ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI
LIWEZE KUENDELEA KULINDA USALAMA WA RAIA PAMOJA NA MALI ZAO KATIKA MKOA
WETU WA MWANZA.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.
Comments
Post a Comment