CCM wampata mgombea ngazi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri-Bukombe

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe na Diwani wa Kata ya Busonzo Mhe. Safari Nikas Mayala(Katikati), Doto Mashaka Biteko(Mb) na  Katibu wa CCM(W)Bukombe Aveline Ngwada wakiwa katika uchaguzi wa kumpata mgombea wa CCM ngazi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe baada ya aliyekuwepo kumaliza muda wake. 




 Waheshiwa Madiwani wakiwa katika uchaguzi wa kumpata mgombea wa CCM ngazi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe baada ya aliyekuwepo kumaliza muda wake. 

 
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na Waheshimiwa Madiwani katika ukumbi wa ofisi ya CCM Wilaya walipokutana kwa ajili ya uchaguzi wa kumpata mgombea wa CCM ngazi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe baada ya aliyekuwepo kumaliza muda wake. 
 Mgombea aliyesimama kujinadi ambae ni Diwani wa Kata ya Lyambamgomgo Mhe. Shitobelo.
 Huyu ni  Mgombea aliyejitoa katika kinyang'anyilo hicho  ambae ni Diwani wa Kata ya Ushirombo Mhe. Lamech Warangi.
  Mgombea aliyesimama kujinadi ambae ni Diwani wa Viti Maalum na aliyemaliza mda wake akiwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe Mhe. Leokadia Kasase
 Katibu wa Madiwani na Diwani wa Kata ya Igulwa Mhe. Richard Mabenga akiwaonyesha wapiga kura na wagombea sanduku la kutunzia kura likiwa halina kitu.
   Katibu wa CCM(W)Bukombe Aveline Ngwada na Mkurugenzi wa Uchaguzi huo akigawa karatasi za kupigia kura.
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akitumbukiza kura yake kwenye kisanduku cha kuhifadia kura.
  Katibu wa CCM(W)Bukombe Aveline Ngwada na Mkurugenzi wa Uchaguzi akifanya zoezi la kuhesabu kura huku wagombea wakipokea kura zao wakati mgombea mmoja ambae ni Diwani wa Kata ya Lyambamgongo Mhe. Shitobelo akiwa amamtumia wakala ambae ni Diwani wa Kata ya Bulangwa Mhe. Yusuph Mohamed kwa ajili ya kusimami kura zake.
Wagombea wakiwashukuru wapiga kura wao baada ya kupatikana mshindi ambaye ni Diwani wa Viti Maalum kwa kura 14 na kuFuatiwa na Diwani wa Kata ya Lyambamgongo Mhe. Shitobelo kwa kura 8

Comments