
Jacob Zuma.
Wabunge
nchini Afrika Kusini leo wanatarajia kupiga kura ya siri ya kuamua
kuhusu hoja ya kutokuwa na imani na Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma.
Baleka
Mbete ambaye ni spika wa bunge hilo amefikia uamuzi huo mara baada ya
vyama vya upinzani kufungua kesi mahakamani wakitaka ipigwe kura ya siri
dhidi ya Rais wa nchi hiyo ya kutokuwa na imani naye.Aidha, Wabunge hao
wanaamini kwamba iwapo kura ya siri itapigwa, basi wabunge wa chama
tawala cha African National Congress (ANC) ambao wanampinga Zuma
watakuwa na uhuru wa kupiga kura dhidi ya rais huyo.Chama cha ANC,
ambacho kimetawala Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi
wa rangi wa Wazungu mwaka 1994, kina idadi kubwa ya wabunge katika
bunge la nchi hiyo.
Hata
hivyo, hili ni jaribio la hivi karibuni la kutaka kumuondoa madarakani
Rais Zuma na linatokea mara baada ya kumfukuza kazi waziri wa fedha
aliyekuwa anpendwa sana na wabunge wengi, Pravin Gordhan pamoja na
mawaziri wengine katika mabadiliko yake kwenye baraza la mawaziri mwezi
Machi.
Comments
Post a Comment