MSHAMBULIAJI
Alexis Sanchez ataukosa mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu ya England kutokana
na maumivu ya tumbo.Akiwa amechelewa kujiunga na wenzake kwa maandalizi
ya msimu mpya kutokana na kuwa na timu yake ya taifa, Chile kwenye
michuano ya Kombe la FIFA la Mabara, Sanchez hataweza kucheza mechi
dhidi ya Leicester City Ijumaa.Lakini Arsene Wenger amesema mchezaji
wake huyo nyota yuko nje kutokana na maumivu. "Ana maumivu madogo
tumboni aliyoyapata kwenye mazoezi ya Jumapili asubuhi kabla hajaja
Wembley,".
"Alifanyiwa
vipimo siku mbili zilizopita na atakuwa nje kwa muda fulani - sifahamu;
wiki mbili au wiki moja zaidi? Lakini hatakuwepo. Nafikiri hatacheza
Stoke. Kwetu, Alexis Sanchez ni pigo" alisema Wenger.
Alipoulizwa
kama Sanchez, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake atasaini
mkataba mpya, Wenger alisema: "Wakati wote inawezekana. Mchezaji
anapokuwa katika mwaka wa mwisho (wa mkataba wake) wakati wote
tutajaribu kumuongezea," alisema. "Hakuna sababu ya kutofanya hivyo.
hatujafika huko bado,"alisema.
Comments
Post a Comment