DOTO BITEKO AWASIHI VIJANA WA MSONGA KUFANYA KAZI BILA KUJALI ITIKADI ZAO


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akifanya shunguli ya kuranda mbao kwenye moja ya ofisi  kijiwe maarufu maeneo ya Msonga  alipowasili kwa ajili ya kuzungumza na mafundi hao 



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mhe. Safari Nikasi Mayala akizungumza na mafundi hao
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na mafundi sermala hao maeneo ya Msonga Kaya ya Runzewe Mashariki
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisindikizwa na baadhi ya mafundi baada ya mazungumzo



Jamii hasa vijana wemeombwa kuacha kufanya siasa za tangu januari hadi desemba bila tija na badala yake wajiunge katika vikundi kwa pamoja bila kujali itikadi,dini wala ukabira wao ili waweze kusaidiwa na serikali kwa haraka zaidi hatimaye  kujipatia kipato kihalali .

Hayo yalisemwa leo na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko alipofanya ziara kwenye Kata ya Runzewe Mashariki na kuzungumza na baadhi ya vijana wanao jihusisha na ufundi seremala  na kusikiliza changamoto zao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mhe. Safari Nikasi Mayala  alisema, haikubaliki vijana na jamii kutumika katika mambo ya ovyo badala ya kujenga taifa, hali ambayo inayowasababishia vijana wengi kutokufanya kazi na kuranda mitaani kwa kisingizio cha kuisubiri serikali iwaletea maendeleo bila wao kushiriki chochote.

Nae Mwenyekiti wa Mafundi seremala hao Alex Gervas amshukuru sana Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb) kwa ujio wake na kumweleza changamoto na uhitaji wa mafundi seremala hao ikiwa ni pamoja na kupanda kwa ushuru wa vitanda  kutoka elfu kumi na mbili ya awali hadi laki moja elfu mbili kwa sasa hali inayowasababishia kutofuanya uzalishaji mkubwa kutokana na changamoto hiyo.
Pia walimuomba Mbunge Doto kuwasaidia ili waweze kutambulika kisheria sambamba na kupata vyeti vya VETA.

Comments