TUCTA YAOMBA WENYE VYETI FEKI WALIOKARIBIA KUSTAAFU WALIPWE MAFAO

Image result for rais wa tucta 2017

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) wamemuomba Rais John Magufuli kuangalia upya watumishi waliokutwa na vyeti feki ambao wamebakisha mwaka mmoja kustaafu waweze kulipwa mafao yao.

Itakumbukwa hivi karibuni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa hakuna mafao kwa waliobainika kutumia vyeti feki.

Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari. Nyamhokya alimpongeza Rais kwa kusimamia vizuri zoezi hilo hivyo wanamuomba kuwafikiria watumishi waliobakiza mwaka mmoja kustaafu walipwe mafao yao ili kukabiliana na ugumu wa maisha waliokuwa nayo.

Comments