Timu zikisikiliza maelekezo kabla ya mchezo kuanza yaliyokuwa yakitolewa na Katibu wa Chama Cha Mpira Wilaya ya Bukombe (BUFA) bw. Bosco Mwidadi
Timu ya Butinzya Fc wakipeana mikono na meza kuu baada ya kumaliza mchezo
Kiongozi wa Timu ya Butinzya Fc akipokea zawadi ya mpira mpya kabisa kutoka kwa Mhe. Diwani wa Kata ya Butinzya Mhe. Amos Shimo ikiwa ni zawadi ya mshindi wa pili katika fainali hiyo.
Timu ya Silamila Fc wakipeana mikono na meza kuu baada ya kumaliza mchezo
Kiongozi wa Timu ya Silamila Fc akipokea zawadi ya Jezi mpya kabisa kutoka kwa Mhe. Diwani wa Kata ya Butinzya Mhe. Amos Shimo ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza katika fainali ya Doto Cup 2017 ngazi ya Kata-Butinzya.
Kama kawaida yetu mashabiki baada ya Ushindi na kujionea zawadi mubashara.
Timu ya Silamila Fc
iliyopo Kata ya Butinzya Wilayani Bukombe Mkoani Geita jana imejinyakulia zawadi ya Jezi mpya ikiwa ni zawadi kwa
mshindi huyo kwa ngazi ya Kata katika Ligi ya Doto Cup 2017 baada ya kuichapa gori 3-0 Timu ya Butinzya Fc katika hatua ya fainali iliyohitimishwa hapo jana katika uwanja wa Shule
ya Sekondari Butinzya.
Mechi hiyo
iliyohudhuliwa na mamia ya mashabiki katika uwanja wa Shule ya Sekondari
Butinzya Timu ya Silamila ilichapa gori 3 Timu ya Butinzya Fc kupitia
kwa Nzala Nangi,Benjami Dominiko na kiungo mshambuliaji Roja Charz.
Hadi dakika tisini ya
mchezo huo Timu ya Butinzya fc haikupata hata gori la kufutia chozi.
Wakati akifungua mchezo
huo Katibu wa Chama Cha Mpira Wilaya ya
Bukombe (BUFA) bw. Bosco Mwidadi ilisema
Akizungumza wakati wa
kukabidhi zawadi hizo, Diwani wa Kata ya
Butinzya Mhe. Amos Shimo alizishukuru timu zote kwa ushiriki wao na kuelezea alichojifunza katika Ligi hiyo ya Doto Cup 2017
Comments
Post a Comment