
Shaffih Dauda.
Mtangazaji
wa Clouds Media Group, Shaffih Dauda ametangaza kujitoa rasmi katika
kinyang’anyiro cha kuwania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) kufuatia tuhuma za rushwa zinazomkabili.
Shaffih
ambaye ni mmoja wa wachambuzi maarufu wa soka nchini ametangaza uamuzi
huo mapema leo asubuhi Julai 28 wakati akizungumza kupitia kipind cha
Clouds 360 kinachorushwa na Clouds Tv.
Akieleza
sababu za uamuzi huo, Shaffih amesema kuwa imekuwa ni kazi ngumu ya
miaka mingi kuweza kulijenga jina lake hadi kufikia hapo alipo leo,
hivyo hawezi kuacha tuhuma hizo za rushwa zinazomkabili sababu ya
uchaguzi wa TFF ziendelee kumchafua.
“Nimetumia muda mrefu kujenga brand yangu hakuna haja kuendelea kung’ang’ania. Suala la Rushwa ni kunichafua na mimi sitaki,” alisema Shaffih.
Uamuzi
huu umekuja ikiwa ni siku chache tu tangu alipokamatwa na kuhojiwa na
TAKUKURU yeye na wenzake kwa tuhuma za kupanga kufanya vitendo vya
rushwa jambo ambalo alilikanusha vikali.
Shaffih
alisema alikuwa kwenye kikao na viongozi wa soka Mkoa wa Mwanza, Mbeya
na wengine wa jirani kwa sababu wanataka kuanzisha michuano ya Ndondo
Cup katika mikoa hiyo, na si kweli kwamba walikutana kwa ajili ya suala
la uchaguzi wa TFF.
Comments
Post a Comment