Michuano ya Doto Cup 2017 yazidi kurindima

Timu ya Ushirombo Fc wakiwa tayari kupambana na mahasimu wao Bulangwa Fc katika kiwanja cha Shule ya msingi Ushirombo ikiwa ni mwendelezo wa Ligi ya Doto Cup 2017.
Hawa ni Bulangwa Fc wakiwa tayari kushiriki Doto Cup 2017 katika kiwanja cha Shule ya msingi Ushirombo dhidi ya Ushirombo Fc 






Ikiwa ni mwendelezo wa Ligi ya Doto Cup 2017 kwa upande wa Kata ya Namonge makeke ya hali ya juu ya  Timu ya Silabela  fc imeisababishia gori 4-0 timu ya Nasiluluma fc kupitia wafunguji mahili ambao ni Emanuel John gori na Hamis Petro gori mbili na hatimae kuibuka kidedea katika mchezo huo.



Kata ya Lyambamgongo vumbi lilitimuliwa na timu mbili za vijiji tofauti kati ya Kagwe Fc na Ishololo Fc huku upande wa Ishololo kuibika mshindi. 



Upande wa Timu ya Bugando Fc ulikuwa msiba mzito baada ya kupokea kichapo cha mbwa mwizi gori sita kwa yai la mbuni dhidi ya Nyamakunkwa Fc.



Haitoshi Kata ya Bulega katika mchezo wa nne wa robo fainali unaononeshwa na kauli mbiu inayosema ‘KUSEMA NA KUTENDA’ ulikutanisha miamba wawili Shilabela Fc na Kivumo Fc na Shilabela kuinuliwa na kiungo wao mshambuliaji Juma kwa kuipatia magoli matatu yaliofungwa dakika ya 60,72 na 84 na mpaka kipyenga cha mwisho cha mwisho kikipulizwa Shilabela Fc 3 na Kivumo Fc 0.



Pia Kata ya Katente mchezo baina ya Ushirombo Rangers na Katente United na hatimae Ushirombo Rangers kuibuka mshindi kwa kijipatia magori matatu huku magori yote yakifungwa na Caroli Francis



Timu ya Ushirombo Rangers na Katente United wakiwa katika picha ya pamoja viongozi wao baada ya kumalizika mchezo na hatimae kuibuka mshindi dhidi ya mahasimu wao Katente United.

 Kilichosemwa na Kocha wa Timu ya Ushirombo Rangers baada ya ushindi
.

Comments