![]() |
Imefungua
kesi hiyo dhidi ya mkuu huyo wa wilaya kwa kuwa ndiye anayedaiwa kushiriki
uharibifu wa miundombinu ya shamba la mbogamboga inalolimiliki wilayani Hai,
Mkoa wa Kilimanjaro.
Kesi
hiyo ambayo iko chini ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Aishael
Sumari, ilifunguliwa Juni 30, mwaka huu na Kampuni ya Uwakili ya D’ Souza&
co ya jijini Arusha kwa niaba ya kampuni hiyo.
Kesi
hiyo ina mashauri mawili ambayo ni shauri la ardhi namba 20/2017 na maombi
madogo namba 51/2017.
Maombi
hayo madogo namba 51/2017, yaliletwa kwa hati ya dharura ambapo mdai anaomba
zuio la muda liweze kutolewa dhidi ya mdaiwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Hai
asiweze kufanya chochote katika eneo la shamba la hekari 2.7 lililopo katika
Kijiji cha Nshara, Kata ya Machame Kaskazini, wilayani Hai, Mkoa wa
Kilimanjaro.
Aidha,
katika kesi hiyo, madai ya msingi ni zuio dhidi ya mdaiwa na wafanyakazi au mtu
yeyote asiweze kuingilia eneo husika, mdaiwa aombe radhi kwa vitendo
alivyovifanya ikiwa ni pamoja na kulipa fidia ya Sh milioni 549.3 kama hasara
aliyoipata mlalamikaji.
Comments
Post a Comment