
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga.
KIBITI:
Hofu kubwa imetanda kwa wagonjwa na wauguzi wa Hospitali ya Mchukwi
iliyopo Kijiji cha Songa, Kibiti mkoani Pwani, ambayo majeruhi
wanaotokana na uhalifu unaoendelea katika maeneo ya Ikwiriri, Kibiti na
Rufiji wanatibiwa.Kwa mujibu wa wauguzi hao, walioomba hifadhi ya
majina yao kwa kuhofia usalama wao, kitendo cha kuwaweka majeruhi hao
hospitalini hapo ni hatari kwao na hata wahudumu wenyewe, endapo wauaji
hao wataamua kwenda kuwamalizia baada ya kuwakosa huko majumbani.Hawa
watu wanafanya mauaji kwa malengo ambayo hayafahamiki, sasa tunahofia
ipo siku watataka kuja kuwamalizia hapahapa, sijui itakuwaje maana hata
sisi sasa tuna hofu kubwa sana, hatuna ulinzi kwa hiyo wakija
watatuokota tu kama kuku,” alisema muuguzi huyo.
Licha ya
kilio cha usalama wao, pia wauguzi hao walisema kitu kingine
kinachowapa tabu ni kukosekana kwa mawasiliano ya simu, kwani eneo hilo
halina ‘network’ kwa muda mwingi.
Akizungumzia
hilo, mmoja wa wauguzi hao alisema licha ya eneo hilo kuwa na wakazi
wengi wanaohitaji huduma ya mawasilino ya simu, lakini hali ni ngumu
sana.
“Sasa kwa
mfano hata kama wakija hapa hao wahalifu, itachukua muda mrefu sana
kupata msaada kwa sababu hatuwezi kupiga simu kwa wakati.
“Inafikia
wakati tunataka kumpa mgonjwa rufaa ya kuelekea Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili au hospitali nyingine, lakini tunashindwa kufanya mawasiliano
na huko tunakotaka kumpeleka.
“Wakati
mwingine tunahitaji kutuma nyaraka mbalimbali za kikazi kupitia
mitandao au kwa kuwasiliana na madaktari wa sehemu nyingine, lakini
hilo nalo linakuwa gumu kwa ajili ya kusaidiana mawazo lakini hilo nalo
linakwama.
“Tunaziomba
kampuni za simu zituletee huduma huku jamani, maana hata ukiachana na
hii hospitali huku kuna watu wengi wanaohitaji huduma ya mtandao,”
alisema muuguzi huyo.
Vitendo
vya mauaji ya raia na viongozi wa vijiji na serikali za mitaa
vinaendelea kutikisa katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani
Pwani na hivyo kuwa tishio kubwa kwa wananchi.
Comments
Post a Comment