Gerard
Pique akiifungia bao la ushindi Barcelona dakika ya 50 ikiilaza 3-2
Real Madrid katika mchezo wa kirafiki wa Kombe la Mabingwa wa Kimataifa
usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Hard Rock mjini Miami, Marekani. Mabao
mengine ya Barca yalifungwa na Lionel Messi dakika ya tatu na Ivan
Rakitic dakika ya saba, wakati ya Real yamefungwa na Mateo Kovacic
dakika ya 14 na Marco Asensio dakika ya 36.
Comments
Post a Comment