Abiria
zaidi ya 100 waliokuwa wakitumia kivuko cha MV Nyerere kutoka Ukara
kwenda Bugorora wamekwama kwenye maji ya Ziwa Victoria baada ya kutokea
hitilafu kwenye Injini ya kivuko hicho na kuzimika.
Mbunge
wa Ukerewe, Mheshimiwa JOSEPH MKUNDI ni miongoni mwa abiria waliokwama
majini baada ya kuzima Injini ya kivuko hicho ameiambia Radio One
kwamba abiria wamekwama kwa zaidi ya saa mbili.
Kuzima ghafla kwa kivuko hicho kilichokuwa na abiria pamoja na magari kunaleta wasi wsi kwa abiria na watu wa neo hilo.
Mbunge
huyo wa Ukerewe amesem tatizo la kuvuko hicho amelieleza mara nyingi
kwa mamlaka husika na wataalam wanasema kinahitaji kuwekwa Injini mpya
ili kifanye kazi ipasavyo.
Habari
za hivi karibuni zinasema abiria waliokwama kwenye kivuko hicho
hatimaye wamefika salama Bugorora baada ya boti kadhaa kwenda kukivuta
kivuko hicho hadi bandarini.
Comments
Post a Comment