![]() |
WATU 16 wamefariki kwenye ajali
ya ndege ya jeshi kwenye jimbo la Mississipi nchini Marekani.
Ajali
hiyo ilitokea katika kaunti ya LeFlore karibu kilomita 160 kusini mwa mji mkuu
wa jimbo hilo, Jackson.
Watu
wote 16 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia ambapo Hakuna taarifa rasmi
zilizotolewa kuhusu kilichosababisha kutokea ajali hiyo.
Kwa
mujibu wa jarida la jimbo la Mississipi ni kuwa ndege hiyo ilianguka katika
shamba moja na mabaki yake yakatapakaa mbali.
Comments
Post a Comment