Trump na Putin uso kwa uso wiki ijayo

Trump na Putin walikubaliana kufanya kazi pamoja siku za nyuma
Trump na Putin walikubaliana kufanya kazi pamoja siku za nyuma

Ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa Rais Donald Trump atakutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wiki ijayo, ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani (G20).
Itakuwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana baina ya viongozi hawa wawili.
Mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani H.R. MacMaster amesema bado hakuna mada maalumu iliyopendekezwa.
Mapema msemaji wa ikulu ya Kremlin alithibitisha uwepo wa mkutano huo. BBC

Comments