Sherehe ya Kula Nyama ya Mbwa Yafanyika China

Sherehe ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika mji wa Yullin nchini China imeanza licha ya ripoti za awali kwamba ilikuwa imepigwa marufuku mwaka huu.

Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Guangxi.

Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa.

Lakini wamiliki wa vibanda vinavyouza nyama hiyo walisema  hawajasikia lolote kuhusu hatua hiyo kutoka kwa maafisa. Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa wa mji walithibitisha kwamba hakuna marufuku yoyote.

Siku ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin zilisema kuwa mbwa waliokufa walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za nyama katika vibanda ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo.

Credit: BBC

Comments