Rais
John Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles
Mwijage, kuwanyang’anya viwanda wamiliki ambao wameshindwa kuviendeleza.
Ameyazungumza hayo leo (Alhamisi) akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambako amezindua viwanda saba.
“Kipindi
cha nyuma tulipofanya makosa ni pale tulipouza viwanda kwa watu
binafsi, sasa kuna viwanda 197 vimeshakufa waliouziwa
hawajishughulishi na vingine vipo kama magofu,” amesema.
Kutokana
na hilo, Rais amesema; "natoa wito kwa wote waliouziwa viwanda kipindi
cha nyuma na sasa wameshindwa kuviendeleza , naagiza sasa basi mrudishe
na wewe Waziri Mwijage tumia hata nguvu kama kuwaweka ndani weka tu
siku akitoka huko atakuta kiwanda kimeanza kazi."
Comments
Post a Comment