Jeshi
la Polisi Dar limekutana na Waandishi wa Habari na kutolea ufafanuzi
mambo mbalimbali yaliyojiri na moja kati ya mambo hayo ni swala la
Walemavu waliotawanywa kwa mabomu ya machozi baada ya kuziba Barabara ya
Sokoine June 16, 2017 wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa.
Jeshi
hilo limesema kuwa halikutumia nguvu kupita kiasi kama inavyodaiwa
lakini walitumia nguvu kulingana na watu waliokuwa wakifanya maandamano
hayo.
"Hatujatumia nguvu ya kupita kiasi. Tumetumia nguvu kulingana na hali ya watu ambao walikuwa wanafanya maandamano hayo.
"Ulemavu, nataka nitoe rai kwa wananchi ulemavu sio kibali cha wewe kuvunja sheria wala ulemavu haukupi wewe kibali cha kuvunja sheria za nchi. Sheria za nchi zipo kwa mtu yeyote yule – mzima au mlemavu na hasa ambaye anazivunja kwa makusudi akijua.
“Hawa walemavu walifanya makosa, wamevamia Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa lakini pamoja na hivyo wakaziba njia. Tumejaribu kuongea nao kuwasihi kwamba wafungue njia lakini pia wateue viongozi wao kwenda kushughulikia matatizo yao lakini walikaidi. Kwa hiyo, ikabidi tutumie nguvu kidogo tukaenda kuwaondosha tukafungua barabara na wananchi wengine wakaendelea na shughuli zao.”
Hayo
yalisemwa jana na Naibu Kamishna wa Polisi ambaye ni Mkuu wa
Operesheni za Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lakini kwa sasa
anakaimu nafasi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Lucas Mkondya alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu kazi
mbalimbali ambazo zimefanywa na jeshi hilo.
Comments
Post a Comment