Uongozi
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umemtia mbaroni kijana mmoja
aliyekuwa akijifanya daktari na alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwa
jina la Dkt. Abdallah Juma.
Aidha,
kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu ya Hospitali
hiyo huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa
akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.
Baada
ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini
kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa
akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na
askari wa hospitali hiyo.
Hata
hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa
Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati
mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni
madaktari kama huyo ambaye alikamatwa jana.
Comments
Post a Comment