Tarehe 22 June 2017, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilipia VIUADUDU
vya kutokomeza Mbu wa Malaria lita 100,000 na kuagiza vigawanywe kwenye
Halmashauri zote nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu anapenda kuwatanganzia
Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwa VIUADUDU hivi vitaanza
kugawiwa leo kwa Halmashauri za Mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha
Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria. Mikoa hii (na kiwango cha maambukizi
ya malaria kimeonyeshwa kwenye mabano) ni;- Kagera (41%), Geita (38%),
Kigoma (38%), Ruvuma (23%), Tabora (20%), Mtwara (20%), Mara (19%),
Morogoro (14%), Shinyanga (17%), Lindi (17%), Pwani (15%), Mwanza (15%),
Katavi (14%) na Simiyu (13%),
Mikoa mingine ambayo haijatajwa itagawia Viuadudu katika Awamu ijayo./
Idadi ya Lita zitakazogawanywa kwa kila Halmashauri zilizo katika Mikoa hii tayari imeshaainishwa.
Wizara inawakumbusha Waganga Wakuu wa
Mikoa/Wilaya kufanya Upuliziaji wa Viuadudu kwa kuzingatia Miongozo ya
Wizara ya Afya. Hii itawezesha kupata matokeo tarajiwa ya kutokomeza mbu
ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini.
Aidha, Wizara ya Afya inapenda
kumshukuru kwa dhati na kumpongeza Mhe.Rais Dkt. Magufuli kwa kuongeza
chachu katika Mapambano dhidi ya Malaria Nchini.
Imetolewa na;
Catherine Sungura
Kaimu Msemaji- Idara Kuu Afya
26 June 2017
Comments
Post a Comment