
Katibu mkuu KKKT dayosisi ya Iringa Nayman chavala akizungumza na wanahabari
Na Fredy Mgunda, Iringa
KANISA la kiinjili la kilutheri Tanzania
(KKKT) dayosisi ya Iringa limesema maandalizi ya kumwingiza kazini
askofu mteule litafanyika jumapili huku likimpongeza Rais Dkt John pombe
Magufuli kwa utendaji kazi.
Katibu mkuu wa KKKT dayosisi ya Iringa Nayman Chavala ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa Kwa wanahabari
kuhusu maandalizi yaliyofikiwa ya sherehe kubwa ya kuwekwa wasifu kwa
askofu mteule Mchungaji Blaston Gavile na msaidizi wake Mchungaji Himidi
Saga.
Alisema kuwa sherehe za kumpa madaraka
ya kuanza kufanya kazi kama askofu wa kanisa la KKT Jimbo la Iringa
mchungaji Gavile na msaidizi wake Saga itafanyika jumapili ya june 25
mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi kwenye viwanja vya shule ya msingi
Gangilonga .
Kuwa ibada hiyo itaongozwa na askofu
mkuu wa KKKT Dkt Frederick Shoo pamoja na askofu mstaafu Dkt Owdenburg
Mdegella na kuwa kabla ya idaba kutakuwa na maandamano ya wachungaji na
washarika yatakayoanzia usharika wa kanisa kuu hadi Gangilonga.
” Tunaomba wananchi wote na washarika
kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la kihistoria pia tunategemea
kuwa na viongozi mbali mbali wa serikali na wageni mashuhuri kutoka
ndani na nje ya Tanzania”
Chavala alisema maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya tukio hilo kubwa ambalo lilikuwa likisubiliwa kwa shauku kubwa .
Askofu Gavile amechukua nafasi ya
aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Dkt Mdegella ambaye alistaafu kwa
heshima kubwa na kuacha heshima ya aina yake ndani ya KKKT .
Wakati huo huo Katibu huyo amempongeza
Rais Dkt Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ya kuwatumikia
watanzania kwa uadilifu mkubwa na kuwa kazi kubwa kwa watanzania ni
kuendelea kumpa ushirikiano .
Kwani alisema kuwa hatua ya kuwabana
wasio waadilifu pamoja na kupambana na wizi wa mchanga wa dhahabu
(MAKINIKIA) ni hatua ya kupongezwa kwani suala hilo lilikuwa
likiwanufaisha wachache huku Taifa likibaki patupu .
” Sisi kama kanisa tumekuwa tukimuombea
kila wakati tena kwa kumtaja kwa jina na hatutachoka kuendelea kumuombea
maana kazi anayoifanya ni ngumu ambayo silaha kubwa ni maombi “
Comments
Post a Comment