Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)
Mkoa wa Geita Comrade Adamu Paul Ndalawa amefanya ziara yake ya kwanza Wilayani
Bukombe na kuzungumza na baadhi ya viongozi, watendaji na wanachama wa Chama
cha Mapindizi (CCM) wa Wilaya ya Bukombe.
Katika ziara hiyo Bwn. Ndalawa
amewaeleza kuwa ni wakati wa wanaCCM hao kubainisha nini vipaumbele vyao katika
kusukuma maendeleo ya Wilaya ya Bukombe.
Moja ya vibaumbele vya wanachama hao
kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Geita Comrade Adamu Paul Ndalawa
ni kuendelea kujenga umoja wa wanachama
na jumuiya zake kwa vitendo na kumhakikishia kupata Hati miliki ya eneo la
ofisi hiyo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bukombe bila kuchelewa.
Aidha kwa upande wake Katibu wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Geita Comrade Adamu Paul Ndalawa amewasihi
wanachama hao kujenga tabia ya kushirikiana kwa umoja ili chama kiendelee kuwa
na nguvu na kuwahamasisha kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama
huku akiwaonya wasimamizi wa uchaguzi kutojenga tabia ya kubagua watu wa
kugombea kulingana na makundi au ujamaa walionao ili kunusuru maslahi ya chama
na taifa kwa ujumla.
Comments
Post a Comment