
Kwa
kawaida wanyama hurahisisha maisha ya binadamu kwa kuwa walinzi, chakula
na usafiri, lakini kuna baadhi ya wanyama na ndege walioweza kujiwekea
heshima duniani hasa kwenye sekta maalum za kijeshi na wameweza kupata
nafasi za juu jeshini.
1: Sir Nils Olav
Nils Olav
ni ndege aina ya Penguin aliyepewa cheo mara ya kwanza mwaka 1972 na
kuwekwa kwenye timu ya walinzi wa mfalme Harald V Loudon wa Norway. Kwa
sasa Sir Nils Olav ni Brigedia anapewa heshima zote za kijeshi ikiwemo
kupigiwa saluti na kukagua jeshi.

2: Treo
Ni mbwa
aliyetumikia jeshi la Uingereza kuanzia mwaka 2001 mpaka 2015. Trio ana
medali zisizopungua 63 ambazo alipewa baada ya kufaya kazi kubwa ya
kutegua mabomu na kutambua mahali mabomu yalipofichwa.

3: William of Orange.
William
ni njiwa aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uingereza mwenye namba MI14
ambapo mwaka 1944 alipewa medali ya 21 baada ya kupeleka ujumbe uliookoa
vifo vya zaidi ya wanajeshi 2000 kwenye vita ya Arnhem wakati wa Vita
ya Pili ya Dunia.

4: Taffy IV.
Huyu ni
mbuzi aliyetumikia jeshi la Uingereza tangu mwaka 1775 ambaye
alichukuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1774 na kuingizwa kwenye jeshi
maalum la Uingereza alipokutwa anarandaranda porini. Alipewa medali ya
14 ambayo ni maalum waliyopewa wanajeshi wa Uingereza wakati wa Vita ya
Kwanza ya Dunia (WWI).

5: LIN WANG
Ni tembo
aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la China kuanzia mwaka 1942 ambapo
alitumika kujenga majengo marefu ya jeshini, kusafirisha chakula wakati
wa vita na alitumika kama kivutio kwa ajili ya kukusanya fedha wakati wa
njaa kipindi cha vita na kupewa medali 12 za kijeshi.

Comments
Post a Comment