Timu ya Walimu wa Bukombe wakiwa Uwanjani.
Timu ya Walimu wa Chato wakiwa katika picha ya pamoja.
Timu ya Walimu ya Netbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita Vijijini.
Timu ya Walimu ya Nyangw'ale(wenye jezi ya rangi nyekundu na nyeusi) na Chato(wenye jezi ya rangi ya njano na kijivu ) wakiwa pamoja na waamuzi wa mchezo wakisubiri maelekezo.
Mgeni rasmi wa Bonanza la CWT Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na viongozi wengine wakikagua timu tayari kwa kuanza mchezo wa fainali.
Mgeni rasmi wa Bonanza la CWT Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko wakiwa na baadhi ya walimu wa Halmashauri ya Bukombe walioshiki katika Bonanza hilo.
Mgeni rasmi wa Bonanza la CWT Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na viongozi wengine katika meza kuu uwanjani hapo.
Mgeni rasmi wa Bonanza la CWT Mkoa wa Geita na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiendelea na utoaji wa zawadi na makombe kwa washindi.
Timu ya Walimu Chato ilijipatia gori 1-0 dhidi ya Timu ya Walimu
Nyangw’ale katika mchezo wa fainali baada ya mchezaji Sikujua Watsoni wa Timu
ya Walimu Nyangw’ale kujifunga gori katika harakati za uokoaji,
Mechi hiyo ulioudhuliwa na mamia ya washabiki ilifanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Buseresere
Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Mchezo huo ulidaliwa na Chama Cha Walimu(CWT) Mkoa wa Geita kwa
lengo la kuimarisha umoja wa walimu na kuunga mkono kauli ya Makamu wa Raisi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan ya watumishi kufanya
mazoezi.
Kwa upande wa Mpira wa Netibali Timu ya Walimu Geita Vijijini
ilikubali kichapo cha gori 24- 10 kutoka kwa Timu ya Walimu Chato.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo mgeni rasmi Mhe.
Doto Mashaka Biteko amesema bonaza hilo ndio kifaa pekee cha kuwaunganisha na
kuongeza undugu wa kujua kazi yao ni moja ya kuelimisha taifa.
Comments
Post a Comment