Korea
Kaskazini imetoa onyo kwa maadui zake Jumamosi hii kwa kuonesha silaha
zake mpya na nzito kwenye gwaride la kijeshi mbele ya kiongozi wake.
Pyongyang imeonesha silaha zake kadhaa kwa mara ya kwanza zikiwemo zile za kutumika chini ya maji.
Hiyo ni ishara kuwa inaweza kuishambulia Marekani au Ulaya bila shida.
Hatua
hiyo imekuja katika kipindi ambacho Rais wa Marekani, Donald Trump
amekuwa akitweet kuwa kama China haiwezi kukabiliana na mpango wa silaha
za nyuklia wa Korea Kusini Marekani itainunua kesi.
Pia utawala wa nchi hiyo umeionya Marekani dhidi ya mashambulio yoyote inayopanga kufanya dhidi yake.
Gwaride hilo limefanyika kusherehekea miaka 105 ya kuzaliwa kwa babu yake Kim.
Kim
anamshutumu Trump kulichokonoa taifa lake kijeshi kwa mfululizo wa
nyendo za kibabe ikiwemo kutuma meli kubwa ya USS Carl Vinson kwenye
peninsula ya Korea.
Comments
Post a Comment