Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Kata ya Katente Comrade Daniel Machongo akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Bwenda Namba1 katika mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na baadhi ya wadau wa Kata ya Katente waliohudhulia katika mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita,Mhe. Doto Mashaka Biteko
amewataka wananchi wa Mtaa wa Bwenda Kata ya Katente hasa vijana kuachana na siasa zisizo na tija huku akiwasilihi kushiriki katika kujiletea maendeleo kwa ujumla na kwa mtu mmojammoja kutokana na rasilimali walizonazo.
Mhe. Biteko aliyasema hayo kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika Mtaa wa Bwenda Kata ya Katente alipokwenda kuonana na wananchi ili kujadiliana shughuli za maendeleo na kusikiliza kero zao.
Alisema inahitajika nguvu ya pamoja ili kuhakikisha
wana maliza changamoto za eneo hilo, zikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya
barabara, kituo cha Afya, miradi ya maji na kuzorota kwa ufaulu wa wanafunzi na
kuwaomba wazazi kushirikiana na walimu kwa kufuatilia kwa karibu zaidi
maendeleo ya vijana mashuleni.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko
alisema yupo tayari kushirikiana na vijana hao katika kujikwamua na wimbi la
umaskini huku akiwasihi vijana hao na Jimbo zima kwa ujumla kujiunga katika
vikundi na kuwaahidi kuleta milioni hamsini na moja kwa ajili ya kuwainua
vijana kwa kuanzisha na kuboresha shughuli mbali mbali wanazozifanya kwa ajili
ya kujipatia kipato kwa umoja wao bila
kujali itikadi,dini wala ukabila .
Comments
Post a Comment