Mhe. Doto azindua vyumba viwili vya madarasa Shule ya msingi ya Amani-Bukombe



Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na baadhi ya wananchi alipowasili shule ya msingi Amani kwa ajili ya ufunguzi wa vyumba viwili vya madarasa.
 


 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Amani wakiwa katika hali ya utulivu na kuwa mashuhuda kwenye tukio la ufunguzi wa vyumba madarasa ya shule ya yao. 

Baadhi ya walimu waliohudhuria katika tukio hilo la ufunguzi wa vyumba hivyo viwili vya madarasa ya shule ya msingi Amani.


Mmoja ya kikundi kilichoburudisha kwenye wa tukio hilo. 
 


 Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya msingi Amani Bw. Marco Magolanga akizungumza kwenye  uzinduzi huo. 

 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Amani  akisoma risala kwa mgeni rasmi ambae ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mhe. Doto Mashaka Biteko. 

Diwani wa Kata ya Igulwa Mhe. Richard Mabenga akizungumza wakati wa tukio hilo ambae vyumba hivyo viwili vya shule ya msingi Amani ni miongoni mwa shule ndani ya Kata yake.
 


 Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mhe. Doto Mashaka Biteko akiweka jiwe la msingi kwenye vyumba hivyo viwili vya madarasa ya Shule ya Msingi Amani.

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mhe. Doto Mashaka Biteko na baadhi ya wananchi wakiwa ndani ya darasa baada ya ufunguzi.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita Mhe. Doto Mashaka Biteko  amezindua  vyumba viwili  vya madarasa katika shule ya msingi Amani Kata ya Igulwa Wilayani Bukombe vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi,mfuko wa maendeleo wa Kata na fedha zilizotolewa na Mbunge kupitia mfuko wa maendeleo wa Jimbo.

Akizungumza na Wananchi pamoja na walimu wakati wa uziduzi huo aliwaomba  Wananchi kumuunga mkono ilikuhakikisha Wanamaliza tatizo hilo la shule mbili kusomea katika jengo moja na kutoa mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya umaliziaji wa vyumba vingine vya madarasa vilivyokuwa vimesimama kwa muda mrefu  ili kuhakikisha  watoto wanasoma Katika Mazingira mazuri na kupata elimu bora  itakayo wasaidia kuepukana na kuwa vibarua wa mataifa mengine.

Bieko alisema hali ya uandikishaji wa wanafunzi imepanda sana baada ya Serikali kutoa elimu bure na wazazi kufanya uamzi mzuri wa kuwapeleka watoto wao kupata elimu na kuwaomba wananchi kuzidi kujitoa kwa dhadi ili kumaliza changamoto hiyo ya ukosefu wa madarasa katika Shule hiyo hali inayopelekea Wanafunzi kukosa vyumba vya kusomea kutokana na wingi wao.

Nae Diwani wa Kata ya Igulwa Mhe. Richard Mabenga alimshukuru Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb) kwa kujitoa kwake kwa  muda na mali na kuwaomba wananchi kuunnga mkono Mbunge huyo na serikali kwa ujumla kwa kuibua miradi ya maendeleo ili kupunguza changamoto zilizoko kwenye kata hiyo.

Kwa upande wao Wananchi Wa Kata ya Igulwa Bw.Marco Magolanga  na Mstafa Juma  walisema wanampongeza sana Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko na Diwani wa Kata hiyo ya Igulwa Mhe. Richard Mabenga  kwa kujitoa kushirikiana na Wananchi kwa kuwasaidia watoto wao kuepukana na mazingira magumu ya kusomea hali iliyo kuwa ikiwatesa watoto hao.

Aidha Wananchi hao wamemuahidi Mbunge huyo  kushirikiana nae kwa kuchangia maendeleo na kuwawezesha Watoto kukaa na kupata madarasa mazuri yatakayo pelekea watoto kupata elimu iliyo bora na itakayo wasaidia katika maisha yao.

Comments