
Usiku wa
April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatolikia
zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuandikwa kuwa Roma
Mkatoliki na Moni wakiwa studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na
watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama
wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio
la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni, Waziri Nchemba ameeleza kuwa
amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.

“Nimeshtushwa
kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka
zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi
kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani
wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”
Comments
Post a Comment