
Baada
ya mapumziko mafupi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa
April 11 2017 mchezo wa kwanza wa robo fainali kati ya Juventus dhidi ya
FC Barcelona ulichezwa mjini Turin wakati mchezo wa Borussia Dortmund
dhidi ya Monaco ukiahirishwa hadi April 12 saa 19:45 EAT kwa sababu za
kiusalama.

Mchezo
kati ya FC Barcelona dhidi ya Juventus nchini Italia ulianza kuibeba
Juventus kuwa na rekodi ya kutowahi kufungwa na Barcelona katika ardhi
ya Italia, wakiwa wamewahi kutoka sare mara mbili na Barcelona kupoteza
mara mbili wakati mara ya mwisho kukutana ilikuwa Berlin katika mchezo
wa fainali UEFA Champions League 2015 na Juventus akapoteza kwa magoli
3-1.

Juventus
wakiwa Turin katika mji wao na sapoti kubwa ya mashabikiwa wao
wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-0, magoli yakifungwa na
Paulo Dybala dakika ya 7 na 22 na goli la mwisho likafungwa na Giorgio
Chiellini dakika ya 55, Juventus na Barcelona watacheza mchezo wa
marudiano April 19 Nou Camp.
Comments
Post a Comment