Ushirombo Rangers yakubali kichapo toka kwa Nyangw’ale Fc kwenye Nne Bora Ya Ligi Daraja La Tatu Mkoa-Geita

Afisa Utamaduni wa Jiji la Mwanza Bw. Julias Kambarage akikagua  Timu ya Ushirombo Rangers Fc kama mdau wa Michezo Wilayani Bukombe.

 Afisa Utamaduni wa Jiji la Mwanza Bw. Julias Kambarage akiwa na wadau wengine wa michezo Wilayani Bukombe akitoa mawaidha kwa wachezaji kabla ya mechi kuanza.


Afisa Utamaduni wa Jiji la Mwanza Bw. Julias Kambarage akikagua  Timu ya Nyangw’ale Fc



Ikiwa ni mwedelezo wa Ligi Daraja la tatu Mkoa wa Geita(GEREFA) hatua ya nne bora kati ya Timu ya Nyangw’ale Fc iliyoko Wilayani Nyangw’ale na Ushirombo Rangers ya Standi kuu ya Ushirombo mjini ambao kwa mchezo wa leo walikuwa wenyeji wa mchezo.

Timu ya Nyangw’ale Fc ilifanikiwa kuichapa gori 3-0 Timu ya Ushirombo Rangers katika mechi hiyo iliyocheza katika viwanja vya Ushirombo Sekondari Wilayani Bukombe. 

Mechi hiyo iliyohudhuliwa na mamia ya mashabiki katika uwanja huo wa Ushirombo Sekondari. 

 Timu ya Nyangw’ale Fc iliichapa gori la 1 Timu ya Ushirombo Rangers Fc dakika ya 47 kupitia kwa mchezaji Maganda Mchembe,gori la pili ni kupitia kwa mchezaji Shabani Yasin dakika ya 80 na la tatu  lilifungwa na kiungo mshambuliaji Maganda Mchembe ikiwa ni dakika ya 82 ambae pia ndie ailiyefunga na gori la kwanza na kuwapatia ushindi mnono timu hiyo ya Nyangw’ale Fc 

 Kwa upande wao Timu ya Ushirombo Rangers katika harakati za kujikwamua hawakubahatika hata gori la kufutia machozi.

 Akizungumza baada ya mechi kumalizika,  Katibu wa Chama cha Mpira Wiayani Bukombe (BUFA) Bwn. Bosco Mwidadi amezipongeza timu zote zilizocheza leo na kuwasihi Ushirombo Rangers kuzidisha bidii kwenye nafasi zilizobaki katika ushiriki wa Ligi hiyo iliyoandaliwa na GEREFA.

Comments