RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA AFYA WA KENYA KUHUSU TANZANIA KUPELEKA MADAKTARI 500(WASIO NA AJIRA SERIKALINI) KWENDA KUFANYA KAZI NCHINI KENYA

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika mazungumzo na ujumbe kutoka nchini Kenya uliongozwa na Waziri wa
Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa
Mailu kuhusu Tanzania kupeleka madaktari 500 nchini Kenya, Ajira za
Madaktari hao zitatangazwa mara moja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na
zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika
utumishi wa umma au taasisi za serikali) waliomaliza mafunzo kwa vitendo
na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Gavana wa Kisumu County Jack Rangumba ambaye aliambatana
na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa
Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu
aliyeambatana pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu akizungumza na Wanahabari
mara baada ya kumaliza mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana
na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu mara baada ya
kumaliza mazungumzo yao.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akimuelekeza jambo Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu
pamoja na Gavana wa Kisumu County Jack Rangumba kabla hawajaondoka Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Afya Ummy Mwalimu akizungumza kuhusu Kutangaza ajira za Madaktari
wapatao 500 ambao watakwenda kufanya kazi nchini Kenya. Ajira hizo
zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika
utumishi wa umma au taasisi za serikali. PICHA NA IKULU.
Comments
Post a Comment