Mhe. Biteko atoa suluhisho ya madarasa yaliyokwama ujenzi katika Shule ya Msingi Kanembwa

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko,Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Bw. Benjamini Mgeta(kulia) na Afisa Mtendaji wa Kata ya Uyovu Bw. Wiliamu Sahani wakiwa katika Ofisi ya Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kanembwa.

Picha ya baadhi ya waalimu na viongozi wa shule hiyo ya msingi Kanembwa.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko na baadhi ya walimu na viongozi wakiangalia hali ya darasa lilikofikia.



Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiangalia madarasa yaliyokwisha kwama kwa muda mrefu.


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kizungumza na waalimu pamoja na viongozi hao amesema dunia kwa sasa inategemea watu wenye elimu hivyo ni muhimu kushirikiana na serikali kuhakikisha watoto wanapata elimu bora kwa kuwaboreshea miundo mbinu ya majengo.

Pia amewasihi kuanzia  kaimu mwenyekiti wa shule hiyo Bw. Alex Gergori na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kanembwa Mwl. Veronika Mfuru pamoja na baadhi ya viongozi wa eneo hilo kuhakikisha wanafikisha hatua husika ya ujenzi huo ili serikali nayo iweze kumalizia na hatimae watoto waweze kupata madarasa ya kusomea. 

Comments