Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha AMAN cha furahia ujio wa Mhe. Doto

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisikiliza changamoto za watoto  toka kwa mama mlezi wa watoto hao yatima na wanaoishi katika mazingira magumu Bi Jamila Hamis.


 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na mmoja wa watoto hao anaetamani akikua awe kiongozi wa juu serikalini.


 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na baadhi ya watoto hao yatima.


 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko pamoja na mama anaewalea watoto hao Bi. Jamila Hamisi wakiwa na baadhi ya watoto hao yatima kituoni hapo.


 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiangalia maendeleo ya kimasomo kwa baadhi ya watoto hao walioanza kusoma.



Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko ametembelea Kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingiza magumu cha AMANI kilichopo Kata ya Uyovu na Kutoa fedha kwa ajili ya chakula pamoja na vifaa mbalimbali.
Mhe. Doto amesema kuwa jukumu la kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu nila kila mwananchi hivyo jamii inapaswa kijitoa kuwasaidia watoto hao.
Kwa upande wake mama anaewalea watoto hao Bi. Jami Hamisi(Mama Sara) amasema shughuli ya kuwalea watoto hao ameana tangu mwaka 1982  na hadi sasa amesha walea jumla ya watoto 117 na kwa sasa anao 30 na kuiomba serikali na jamii kwa ujumla wake kumuunga mkono kwa kuwasaidia watoto hao ili waweze kupata elimu na hatimae kujitegemea.

Comments