Wafanya Biashara wa Uyovu watoa Changamoto zao kwa Mhe. Doto Biteko

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizumgumza na wafanyabiashara wa Kata ya Uyovu.

 Baadhi ya wafanyabiashara wa Kata ya Uyovu wakizungumza na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.

Mmoja wa wafanyabiashara hao alieuliza maswali katika mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko

 Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Uyovu Dkt John Fabiani Ng'home akizungumza kwenye mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko alipokutana na wafanya biashara wa Kata ya Uyovu nakuwaeleza Kituo hicho cha Afya kinawahudumia wagonjwa wengi hasa wazee,watoto na wamama wajawazito ambao hutibiwa bure na kumwomba Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb) kuishinikiza Serikali kupandisha  Hadhi Kituo hicho cha Afya.



Mkuu wa Kituo cha Polisi Insp. Richard G. Mkesi  akizungumzia masuala ya Usalama Barabarani katika Kata hiyo ya Uyovu na kuwaomba wafanyabiashara hao pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa mabarozi wazuri ili kumaliza suala la uvunjaji wa sheria.



Wafanyabiashara wa Uyovu Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita wamekutana na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko na kumweleza umuhimu wa sekta hiyo na changamoto zao.

Pia wamemweleza Mbunge huyo kuwa pamoja na kuchangia serikali maendeleo kwa kulipa kodi hawanufaiki na fedha zao hizo kutokana na serikali kutotengeneza miundombinu ya barabara hasa  Kitongoji cha Azimio na  huduma ya umeme kufikia watu wachache sana hali inayo wanyima fursa ya kuboresha biashara zao.
Kwa majibu ya Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb) aliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa umeme uliosambaa kwa sasa sio wa mradi wa REA nakusema mradi huo ulikuwa unaitwa UMEME NAMBA 5 uliokuwa unafadhiliwana na Banki ya maendeleo ya Afrika(ADB) na kuwaomba wawe na subira kwani Wilaya nzima na viunga vyake vimeingizwa kwenye mradi wa REA na kuwahakikishia kumaliza changamoto ya umeme kabisa
Pia aliwasihi wafanyabiashara hao kuachana na siasa na badala yake wawe kipaumbele kwa kuibua miradi ya maendeleo ili waweze kupata fedha za ruzuku kutoka serikalini ili kuharakisha maendeleo kwa mmoja mmoja na kwa ujumla.       

Comments