Mkuu wa
wilaya ya Longido mkoa wa Arusha, Godfrey Chongolo akizungumza wakati wa
ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa(Tamisemi), Mh.Suleiman Jaffo(kulia) anayesikiliza kwa makini
na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halamshauri ya Longido, Juma Mhina.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi), Mh.Suleiman Jaffo(kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa
Chama cha Walimu mkoa wa Arusha, Lootha Laizer.
Baadhi ya
Madiwani na watumishi wa halmashauri ya Longido wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi), Mh.Suleiman Jaffo.
Baadhi ya
Madiwani na watumishi wa halmashauri ya Longido wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi), Mh.Suleiman Jaffo.
Naibu
Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi), Mh.Suleiman Jaffo(kulia)akizungumza jambo alipotembelea
eneo linapojengwa soko la kisasa la mifugo katika Kijiji cha Orendeke
Kata ya Namanga mkoa wa Arusha,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Longido,
Godfrey Chongolo.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi), Mh.Suleiman Jaffo akizungumza na wananchi wa Kata ya
Makuyuni wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha baada ya kukagua ujenzi wa
Kituo cha Afya,serikali imetenga kiasi cha Sh 700 milioni kwaajili ya
upanuzi wa Kituo cha Afya Mto wa Mbu.
Muuguzi
katika Kituo cha Afya cha Usa River, Emiliana Sulle(kushoto) na Mganga
Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha, Bonifas
Ukio(kulia) Mh. Suleiman Jaffo kumpima uzito mtoto ili kujua maendeleo
yake.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Mh.Suleiman Jaffo(kulia)akiagana na Mbunge wa jimbo la Monduli,Julius
Kalanga baada ya kumaliza ziara yake mkoani Arusha.
Mwandishi wetu,Arusha
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Mh.
Suleiman Jaffo amewataka watumishi katika halmashauri zote nchini
kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wawe wabunifu katika kutatua
changamoto zinazowakabili wananchi.
Katika
ziara yake mkoani Arusha katika halmashauri za Meru, Longido na Monduli
alisema serikali imeshatoa fedha za Mfuko wa Pamoja wa Afya(Basket Fund)
katika halmashauri hizo hivyo kukosekana kwa madawa na vifaa tiba sio
jambo linaloweza kuvumilika.
Alisema
miradi yote ambayo fedha zimeshaletwa na serikali kuu kwenye halmashauri
itekelezwe mara moja ili iweze kuwahudumia wananchi.
Comments
Post a Comment