HAFLA YA UZINDUZI WA MRADI WA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU (REA III) KATIKA MKOA WA IRINGA.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Nishati Vijijini, Dkt Gideon Kaunda akizungumza na Wananchi
wakati wa Hafla ya uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu
ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Iringa uliofanyika katika kijiji cha
Image wilayani Kilolo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo.
Mkurugenzi
Mkuu wa REA, Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa kwanza kulia), Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia), Mbunge wa
Kilolo, Mhe.Venance Mwamoto (wa tatu kulia) wakisoma maombi ya wananchi
ya kuunganishiwa umeme katika Mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu
ya Tatu, wakati wa Hafla ya uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme
vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Iringa uliofanyika
katika kijiji cha Image wilayani Kilolo.
Wanafunzi
wa Sekondari ya Wasichana wa Jamii ya Kimasai wilayani Kilolo
wakitumbuiza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme
vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Iringa uliofanyika
katika kijiji cha Image wilayani Kilolo.
Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kuli mstari wa
nyuma) pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja kabla
ya kuzindua mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu (REA III)
katika mkoa wa Iringa. Wa nne kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina
Masenza, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Gissima
Nyamo-hanga na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini,
Dkt Gideon Kaunda. Waliosimama mbele ni Wanafunzi wa Sekondari ya
Wasichana wa Jamii ya Kimasai wilayani Kilolo.
Comments
Post a Comment