VITA YA MADAWA YA KULEVYA: ASKARI 12 WALIOTUHUMIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA WASIMAMISHWA KAZI
Kufuatia
tuhuma zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
zikiwahusisha baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi kujihusisha na
biashara ya madawa ya kulevya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP
Ernest Mangu amewasimamisha kazi Askari 12 waliotuhumiwa ili uchunguzi
ufanyike dhidi yao.Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi uliopita,
IGP Mangu alisema ni lazima Jeshi la polisi lichukue hatua kali dhidi
ya yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo, hata kama ni
Askari."Jeshi la Polisi linachukua hatua madhubuti za kuwachunguza
Askari na Wasanii waliotuhumiwa na baada ya uchunguzi kumamilika hatua
za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayethibitika kwa uhalifu huo"
alisema IGP Mangu.Pia IGP Mangu ameiomba jamii kuendelea kutoa taarifa
za uhalifu wa aina yeyote ili nchi iendelee kuwa salama.hapo chini ni
Majina ya Askari wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya
kulevya, ambao wamesimamishwa kazi.
Comments
Post a Comment