Wachezaji wa Timu ya Runzewe Academy wakijadiliana nini kifanyike dhidi ya wapinzani wao.
Mwamzi wa Mchezo akitoa kadi ya NJANO kwa Masanja Sabuka wa Timu ya Runzewe Academy kwa kumfanyia Madhambi Juma Mbelele ambaye ni Mchezaji wa Timu ya Ushirombo Rangers.
Kama kawaida yao Mashabiki.
Baadhi ya Mashabiki wakiwa katika umakini wa kufuatilia Mchezo.
Timu
ya Ushirombo Rangers imeibuka kidedea
dhidi ya Timu ya Runzewe Academy kwa kuichapa gori moja bila kwenye viwanja vya Runzewe Stadium katika
michuano inayoendelea ya ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa inayoratibiwa na Chama Cha Mipira wa Miguu Mkoa wa Geita (GEREFA)
.
Mechi ya kwanza ya timu hizo imechezwa na iliyohudhuliwa na mamia ya mashabiki katika uwanja wa Runzewe Statium ambapo Timu ya Ushirombo Rangers iliichapa gori 1 Timu ya Runzewe Academy dakika ya 82 kupitia kwa kiungo mshambuliaji Nestory Jamhuri.

Hadi
dakika ya tisini ya mchezo huo Timu ya Runzewe Academy haikupata hata gori la
kufutia chozi.
Kipa wa Ushirombo Rangers Fadhili Selemani ndiye aliyekua
nyota wa mchezo kwa kuokoa mipira mingi ya hatari likiwemo shuti la Athony Mwalyoyo alilopiga ndani ya 18 na kipa huyo wa Ushirombo Rangers kuiokoa kwa juhudi kubwa .
Comments
Post a Comment