RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA MSUYA NYUMBANI KWAKE UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya nyumbani kwake Upanga jijini
Dar es Salaam. Waziri
Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu mpaka aliporuhusiwa kurejea
nyumbani kwake mara baada ya kupata nafuu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuombea
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani
kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimsindikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifika nyumbani kwake Upanga
kwa ajili ya kumjulia hali.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani
kwake Upanga jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment