Mfugaji wa nyuki akutana na risasi

Picha ya aliyepigwa risasi (Sizya Emanuel) na Askari wa wanyapori kwenye pori la akiba la kigosi Muyowosi.

Kibali cha kufugia nyuki katika pori la akiba Kigosi Muyowosi

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko ameiomba serikali kutoa suluhu ya kudumu baina ya wananchi wa Bukombe na askari wa wanyama pori katika pori la akiba la Kigosi Muyowosi baada ya kijana mmoja anayejishughulisha na ufugaji wa  nyuki  katika pori hilo  aliyefahamika kwa jina la Sizya Emanuel kupigwa risasi na baadhi ya askari hao kisogoni na kutokezea jichoni.

Wakati akizungumzia tukio hilo, Mhe. Doto ametoa pole kwa familia iliyopata tatizo hilo na kuwasihi askari hao kuwa makini katika utendaji ili matukio kama hayo yasijirudie tena.



 Hii hapa kauli ya serikali kuhusu suala hilo



 

Comments