Mbunge Doto asisitiza maendeleo Narusunguti

 Shule ya Sekondari iliyoko Kata ya Busonzo inayotegemea kufunguliwa.

 Vyoo vya Shule hiyo(picha hapo juu) vilivyofadhiliwa fedha za ujenzi  na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko. 


 Nyumba za Waalimu wa Shule hiyo iliyoko Kata ya Busonzo katika hatua za awali (msingi).
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko pamoja na msafara wake wakiwa katika shule ya msingi Narusunguti kwa ajili ya kupokea changamoto za shule hiyo. 


  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko na msafara wake wakitokea Shule ya Msingi Narusunguti baada ya kuzungumza na waalim pamoja na uongozi wa Shule hiyo. 


  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Narusunguti. 


 Wananchi wa Kijiji cha Narusunguti wakiwa katika umakini zaidi wa kumsikiliza  Mbunge wao


 Hawa ni baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Narusunguti  waliojiteza kuuliza maswali katika mkutano wa Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb).


   Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akimkabidhi mipira mmoja wa waalimu wa Shule hiyo ya msingi Narusunguti baada ya ombi lao.



Mbunge wa jimbo la Bukombe Mkoani Geita,Mhe. Doto Mashaka Biteko
amewaomba wananchi kuacha vitendo vya kuendekeza siasa wakati wa
kutekeleza shughuli za maendeleo zinapo ibuliwa kuanzia ngazi ya Kijiji ili kujiletea mandeleo kwa haraka.

Biteko aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Narusunguti Kata ya Busonzo alipokwenda kuwashukuru wananchi kwa kumchangua na kuhamasisha kuibua
miradi ya maendeleo kwani Wilaya ya Bukombe iko nyuma kimaendeleo
kutokana na wananchi kuendeleza siasa hali ambayo imesasabisha bara
bara nyingi hazijafunguliwa, huduma za Afya zisizo endana na  mahitaji
ya watu  kutokana na upungufu wa Zahanati.

Mbunge aliwaomba wananchi waungane kujitolea kujenga darasa la shule ya msingi Narusunguti na kuwaahidi kuwaletea mabati ya kupaulia darasa hilo ili kupunguza adha ya watoto kusoma katika hali ya mbanano na kuwasababishia kufanya vibaya kimasomo katika mtihani wa darasa la saba kwa kuwa wa tatu kutoka mwisho kati ya shule 75 za Wilayani humo. 

Wakati akibainisha mafanikio kwa Wilaya ya Bukombe kwa sasa alianza kwa kuwapongeza wanaNyarusunguti kwa kumaliza kabisa changamoto ya madawati katika shule hiyo na kuwasihi kuongeza ushirikiano kwa waalimu ili kuongeza ufaulu wa watoto hao.   
Pia aliwasihi wakazi hao kuwajengea utamaduni wa kusomesha watoto wao kwani shule ya sekondari ya Busonzo imekaribia kufunguliwa ili ianze kutoa huduma ya elimu na kutoa fedha kwa ajili ya ujezi wa vyoo ili kuharakisha  uanzishwaji wa shule hiyo.   

Mhe Biteko alisema  kwa kushirikiana na serikali barabara ya Namparahara hadi Msonga itaanza kukarabatiwa hivi karibuni na tayari fedha zimekisha tolewa ili kuboresha miundo mbinu hiyo na kuongeza vituo vya Afya na Zahanati ili kuondoa chamgamoto  za kutembea umbali mrefu kutafuta  huduma za Afya.
 

Awali mkazi wa Kijiji cha Narusunguti Nduta Ngasa  alisema kuwa kutokana
na Kata hiyo kutokuwa na huduma muhimu ya shule ya sekondari na
Zahanati  wanafunzi na wananchi wamekuwa wakipata changamoto
ya kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma hizo na kumwomba Mhe. Doto Mashaka Biteko (Mb) kuitatua changamoto hizo za maji katika Kata hiyo ili kuwanusuru wakazi wa maeneo hayo.




Comments