KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA BUKOMBE

 Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekieli Kyunga (wa pili kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Josephat Maganga (wa kwanza kushoto),Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe na Diwani wa Kata ya Busonzo Mhe. Safari Nikas Mayala (katikati) na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko wakiwa katika umakini wa kupitia makablasha ya kikao.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Afya Elimu na Maji Mhe. Juma Lushiku (kushoto) anaemfuata ni Mwenyeki wa Kamati ya maadili Mhe. Lozaria Masokola na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mzingira Mhe. Lameck Warangi

 Baadhi ya Madiwani nao kwa umakini mkubwa wakipitia makablasha.

 Picha ya Baadhi ya Watumishi  katika Wilaya ya Bukombe.

 Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga  akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo la Madiwani.



Madiwani  wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamemuomba Mkuu wa Mkoa Geita  Meja Jenerali Ezekieli Kyunga kuinua wakulima wa mazao ya chakula na biashara kwa kuwasaidia kuwatafutia wadau wenye uwezo wa kuwaletea pembejeo sahihi ili wakulima hao waepukane na hasara zitokanazo na dawa zisizoweza kuuwa wadudu waharibifu wa mazao,

Sambamba na kumwomba Mkuu huyo kuzidisha mkuzo kwa kushilikiana na Wakuu wa Wilaya katika kuhakikisha Chakula hakiuzwi nje ya Mkoa wa Geita kutokana na kuzidi kwa ukame katika msimu wa mwaka huu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya  Madiwani hao Mhe. Eric Kagoma na Juma Lushiku wamesema kuwa  wamekuwa wakicheleweshewa pembejeo za kilimo huku zingine zikiwa haziwauwi wadudu hao kabisa hali inayowakwamisha katika uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na kilimo cha mazao.

Katika hatua nyingine Mhe. Lushiku  amemuomba Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kujua idadi halisi ya chakula kilichopo na mahatiji ya watu kwa sasa  na kuviomba  vyombo vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha zao la chakula hali toki nje ya Mkoa.  

Lushiku aliwataka Madiwani  hao kuongeza bidii ya kutoa ushirikiano wa kutosha kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kupunguza matukio mbalimbali ya uharifu yanayoripotiwa kutokana na hali ngumu itokanayo na ukame .

Pia Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mhe. Doto Mashaka Biteko aliwaomba madiwani kutoa elimu kwa wananchi juu uvunjaji wa sheria na kuwasihi watumishi wa idara mbalimbali katika Wilaya hiyo kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi bila ubaguzi na unyanyasaji wa aina yeyote. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Ezekieli Kyunga alisema atahakikisha anatoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wa ngazi zote ili kuleta maendeleo ya Wilaya,Mkoa na Taifa kwa ujumla 

Mhe. Kyunga aliwataka  viongozi hao kuzidisha ubuni na utafiti ili kumaliza changamoto katika jamii ikiwa ni pamoja na kuendeleza ulinzi shirikishi,kujenga maghala ya kuhifadhia chakula kama Wilaya,kujenga tabia ya kufanya biashara baina ya kata na kata, Wilaya na Wilaya ili kuunusuru Mkoa na balaa la njaa.



 


Comments