Kamishna Mihayo aongoza mazishi ya Peter James Kubezya-Bukombe

 Maafisa wa Jeshi la Polisi wakiuweka mwili wa marehamu vizuri tayari kwa kuuaga


 Viongozi wa Dini kwa pamoja wakiuombea mwili wa merehemu.






 Hawa ni sehemu tu ya umati wa waombolezaji.
 Kamishna wa Operasheni ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya, Mihayo Msikela(kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wengine wakiomboleza.





 Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani  akisoma risala.






  Kamishna wa Operasheni ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya, Mihayo Msikela akizungumza na umati wa msiba na kuwatia moyo.

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ikitoa maneno ya faraja kwa waombolezaji.
 
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(W)Bukombe Mhe. Zakaria Bwire akiwakilisha Chama.

 Diwani wa Kata ya Ushirombo Mhe. Lameck Waranngi akizungumza na umati wa msiba.

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe Paul Cheyo akisema neno kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe.

 Mjomba wa marehamu akipokea mchango wa rambirambi toka kwa kiongozi wa umoja wa wafanya biashara- Bukombe.

 Mama wa marehemu akiuaga mwili wa mwanae.
 Mke wa Marehemu akilia kwa uchungu sana wakati wa kuuaga mwili wa mmewe.
 Safari ya kuelekea eneo la maziko.

 Gwaride la Heshma ya Mwisho kwa marehemu.
 Maafisa wa Jeshi la Polisi wakifanya maandalizi tayari kwa kuushusha mwili wa marehemu. 

 Mke wa Marehemu akiweka Taji.
 Kamishna wa Operasheni ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya, Mihayo Msikela akiweka Taji.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akiweka Taji.




 
Kamishna wa Oparesheni ya kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya Ndg Mihayo Msikela ameongongoza mamia ya wananchi wa Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita na Taifa zima kwa ujmla wake katika mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi(Oc Cid) katika Wilaya ya Kibiti Ndg Peter James Kubezya nyumbani kwao Kijiji cha Mwalo Wilayani Bukombe.


Akitoa salamu za jeshi katika umati huo wenye huzuni kubwa alisema familia,jamii na serikali ni pengo kubwa kwa kuondokewa na mpendwa wetu na kuwasihi wananchi kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya kiarifu bila woga ili nchi iendelee kukaa kwa amani kwa kuondoa jamii ya watu wachache waovu na kuwaacha wengi wakiwa na amani na utulivu.


Mazishi hayo yaliyoudhuliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Bukombe pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali za kisiasa,kidini na serikali.
Mhe. Doto Biteko(Mb) amesema kuwa kamwe wanabukombe hawatamsahau kwa ajili ya utu wake,upendo kwa watu na utumishi uliotukuka.

Awali akitoa mahubiri hayo Paroko Fabiani amesema ni wakati wa kupata hofu ya Mungu ili kulinusuru Taifa letu liwe na amani na kuusihi umati kuwatanguliza wenzao katika kutenda mema kama alivyokuwa Peter Kubezya.    


  



 

Comments